Ticker News

Your Ad Spot

Monday, March 2, 2026

DAWA YA JINO SI KULING'OA, ONANA NA MTAALAMU WA AFYA AKUTIBU


Na Khamisi Mussa – Dar es Salaam

Imebainishwa kuwa dawa ya jino bovu si kuling’oa balini kufika hospitali kuonana na wataalamu wa afya ambao watasaidia kutibu na kuwaepusha watu kuwa na ulemavu wa kudumu wa kinywa na meno.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za afya, kinywa na meno kutoka Wizara ya Afya Dkt. Baraka Nzobo wakati akizungumza na waandishi wa Habari na kusema kuwa watu wengi wamekuwa wakichukua hatua za kungoa meno yao bila kufuata utaratibu wa matibabu jambo ambalo ni hatari kwa afya ya kiywa na meno.

Dkt. Nzobo alisema asilimia kubwa ya Watanzania wanasumbuliwa na changamoto za meno hasa meno kuoza kwa muda mrefu lakini hawafiki hospitali kwaajili ya kupata matibabu, inapofikia wanapata maumivu makali ndio wanaenda hospitali hivyo kupelekea kung’olewa jino.

“Dawa ya jino bovu sio kulin’goa jino bovu linatibika, kumekuwa na dhana ya kutokufika hospitali kufanya uchunguzi hivyo kuipelekea jamii kuchukua maamuzi ya kung’oa meno pale yanapouma”, alisema Dkt. Nzobo

Dkt. Nzobo alibainisha kuwa zipo taratibu za kiafya ambazo zikichukuliwa zinaweza kusaidia kuimarisaha afya ya meno badala ya kung’oa.

“Unatakiwa ukifika hospitali na kufanya x-ley ya jino linaloonyesha uharibifu ili kuona ni hatua gani limefikia, baada ya kufanyiwa uchunguzi wataalamu wa afya watakupa ushauri wa nini cha kufanya kama ni kuliziba ama kutumia dawa ili uweze kukaa sawa”, alisema Dkt. Nzoba  

Asilimia zaidi ya 80% ya Watanzania ambao wanachangamoto ya meno kuoza yanaweza yakazibwa vizuri na kupona kabisa na tukabaki na asilimia 10 hadi 20 wale ambao wamechelewa kufika hospitali ndio wanaweza kung’olewa meno.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages